Posts

Showing posts from April, 2025

SIRI NYETI KUHUSU MAHUSIANO BY DOMINICK MWENDA

Image
  Ati ukimwi! Ukimwi sio janga, zinaa (uasherati) ndio janga. Lakini hili leo limekuwa tofauti sana. Watu wamefanya zinaa kuwa kama starehe nyingine tu, lakini kwa kweli zinaa inaua, inaaibisha, inaharibu, inateketeza na inachafua. Kabla hujajitosa katika dhambi ya zinaa, tafadhali jiulize yafuatayo; Ndiyo zinaa ni starehe ya madakika tu, ila;  Huyu ninaye taka kustarehe naye leo, jana alistarehe na nani?    Pengine unampango naye kwenye maisha, labda mje kuwa wanandoa. Je, leo umemshawishi akakubari, vipi kesho akishawishiwa na mwingine?    Pengine ni mme au mke au binti au kijana wa watu, ukifumaniwa si aibu mtaani?    Pengine anamagonjwa sugu ya zinaa, je ukiyapata uko tayri kujitibu?    Pengine leo ukatoa au kupata mtoto uko tayari kumlea?    Ukisalimika kwa yote hayo, je kwa MUNGU utasalimika?   Mahusiano ya kweli Licha ya kwamba watu wanafanya uzinzi na uasherati lakini bado mahitaji ya kuwa na ndoa njema yangalipo. Hakika hakuna ndoa bora...