SIRI NYETI KUHUSU MAHUSIANO BY DOMINICK MWENDA
Ati ukimwi!
Ukimwi sio janga, zinaa (uasherati) ndio janga. Lakini hili leo limekuwa tofauti sana. Watu wamefanya zinaa kuwa kama starehe nyingine tu, lakini kwa kweli zinaa inaua, inaaibisha, inaharibu, inateketeza na inachafua.
Kabla hujajitosa katika dhambi ya zinaa, tafadhali jiulize yafuatayo;
Ndiyo zinaa ni starehe ya madakika tu, ila;
Huyu ninaye taka kustarehe naye leo, jana alistarehe na nani?
Pengine unampango naye kwenye maisha, labda mje kuwa wanandoa. Je, leo umemshawishi akakubari, vipi kesho akishawishiwa na mwingine?
Pengine ni mme au mke au binti au kijana wa watu, ukifumaniwa si aibu mtaani?
Pengine anamagonjwa sugu ya zinaa, je ukiyapata uko tayri kujitibu?
Pengine leo ukatoa au kupata mtoto uko tayari kumlea?
Ukisalimika kwa yote hayo, je kwa MUNGU utasalimika?
Mahusiano ya kweli
Licha ya kwamba watu wanafanya uzinzi na uasherati lakini bado mahitaji ya kuwa na ndoa njema yangalipo. Hakika hakuna ndoa bora iliyotokana na mahusiano mabaya, wala ndoa mbaya iliyotokana na mahusiano mema. Haipo!
Hivyo mtazamo wa kuwa na ndoa bora huja kwa kila mtu, bali mitazamo ya watu wengine, mazingira mtu anayo kulia yanamfanya kuhama katika mtazamo huo, si kwakupenda bali kwa ulazima wa mazingira. Hivyo Subira, uelewa, na uaminifu havinabudi kututawala ili swala hili lisiwegumu tena.
Nje na hayo yote, shetani naye asingekubali kuwa mshuhudiaji tu, hufanya kila namna kuwapiga Watoto wa Mungu. Hivyo, hatima yake sasa ndio hii, kaondoa radha ile ya awali katika ndoa. Na wengine wameingia katika uongo mkuu na kugeuza ngono ndiyo maisha, wakijidanganya na asili ya dunia hii ya sasa. Eti ndoa ni ushamba nakupitwa na wakati! Hakika endeleenikujikuta wakileo, Mungu atawaadhibu.
Wengine wamekuja na kondomu. Hii inaonesha jinsi gani shetani alivyojithibiti katika kupromoti zinaa ulimwenguni. Watu wamekuja na kondomu wakijua yakwamba ndio Suluhu. Pole sana! Zinaa ni zinaa tu. Hakikahainabudi kuepukwa na kila binadamu.
Mambo yote haya yanakuja kwa sababu watu wameamua kumwacha Mungu (kumwona hafai tena). Hakika hayo yakiwa ndio maisha yetu, basi tusahau kwa Habari ya famila bora, ndoa bora, malezi bora, Watoto bora wenye malezi. Na tukifika huko dunia itakuwa uwanja wa fujo,vilio, masononeko na majonzi makuu.
Mahusiano ya kweli hulenga;
Kuanzisha ndoa njema na sio ndoa za mikataba.
Kuwa na mahusiano ya kudumu na sio kwa mpito tu.
Kuchukuliana na kusameheana, kwa maana kuwa katika mahusiano na kudhani kuwa hamtakuja kukosana hata kidogo ni mtazamo unaoweza kuharibu hata mahusiano yenyewe.
Hata hivyo mtu hanabudi kuwa kwanza na mipango, juu ya mtu wa namna gani anataka aolewe naye au kumwoa. Hii itasaidia kuwa mvumilivu pale changamoto inapotokea.
Mahusiano ya kweli hayanabudi ya thibitishwe na Mungu
Katika hatua zote za maisha, hatua ya kwanza haina budi awe Mungu, watu wanaposhindwa kupitia katika hatua hii matokeo yake ndiyo kuharibu na kuaibisha. Mtu yeyote akitaka kuanza safari ya kujiingiza kwenye mahusiano, amshirikishe kwanza Mungu. Kwamaana Biblia haikukosea kusema kuwa mke/(mume) bora hutoka kwa BWANA. Hii ni kwasababu shetani akiisha kutambua mpango ulionao hupanda mbegu za uharibifu.
Tatizo kubwa hapa ni kwamba wapo watu ambao hawaamini katika uwezo wa Mungu, nadharia za kibinadamu, na Mawazo yasiyo na kifani ambayo binadamu huwaza, humfanya amwone MUNGU kuwa kama si mweza hata kidogo. Na mbali zaidi, baadhi ya watu hawaamini hata ya kwamba Mungu ni mweza.
Kudai kwamba hakuna Muumba ni wazo la kipumbavu sawa tu na kudai kwamba, nyumba hii haijajengwa na mtu yeyote.
Hii ni kwasababu shetani akiisha kutambua mpango ulionao hupanda mbegu za uharibifu. Watu wanaposhindwa kumtanguliza MUNGU, huishia kuongozwa na tamaa.
Nguvu ya tamaa katika kufanya maamuzi sahihi.
Tamaa huweza kuwa njema au mbaya, hata hivyo tamaa njema ndizo zinazohitajika. Tamaa njema ni kama;
i. Kutamani kuwa na familia nzuri na inayomcha Mungu.
ii. Kutamani kuwa na mahusiano bora katika kipindi chote cha maisha. Kwasababu mahusiano ni jambo endelevu ambalo hudumu katika kipindi chote cha maisha hapa duniani. Hivyo kuwa na mtazamo wa kutengeneza mahusiano mema hata mwisho ni jambo jema.
iii. kutamani kuwa na Watoto wanaomcha Mungu na wenye msingi wa maadili. Kwasababu nidhamu na maadili ya mtoto wako hutegemea maisha yako ambayo unayaishi sasa. Hivyo kuishi kama unavyotaka Watoto wako wawe ni tamaa njema.
iv. Kutamani kutokuwa na mahusiano na mtu mwingine wakati tayari unamahusiano na mtu. Hii ni tamaa njema sana.
Tamaa zote hizi ni njema, na hazinabudi ziwe malengo ya kila mtu anayetaka kuwa na mahusiano mazuri.
Tamaa iliyo nje na lengo jema ambalo hata Mungu haliungi mkono, ni uzinifu mkubwa.
Jinsi ya kutambua tamaa mbaya;
1. Huwa haina mipaka. Tamaa mbaya haijui wapi iishie na wapi iaanzie.
Badala ya kufikiri jinsi gani mtatengeneza ndoa bora, inafikiri kuhusu tendo la ndoa (ngono).
Badala ya kufikiri hatua za kuibariki ndoa, inafikiri kumwita chumbani mlale wote kabla ya ndoa.
Badala ya kumpenda kwa vile ni mvumilivu, mcha Mungu, mwenye bidii katika kazi, na mna uwezo wa kuchukuliana na kusameheana, inavutiwa tu maumbo ya nje kama pesa, rangi, na umbo.
Badala ya kushirikishana unachokijua kuhusu maisha, unashirikisha kuhusu uzoefu wako kwenye ngono.
2. Huwa haina mipango. Tamaa mbaya haina mipango hata kidogo.
Mmekutana tu kwenye mitandao ya kijamii, tayari unataka kumwoa au kuolewa naye mara moja. Ni tamaa hiyo!
Mmekutana tu kwenye starehe, tayari umeshataka kumwoa au kuolewa naye. Ni tamaa hiyo!
Mmekutana tu kwenye njia tayari unataka kuoa au kuolewa naye. Ni tamaa hiyo!
Hatua;
- Jiepushe kukaa muda mwingi na watu wanaozungumzia mambo ya mapenzi. (cut off fake people for the real reasons and not real people for fake reasons)
- Jifanye uko bize(busy) wakati mwingi.
- Pata muda wa kutafakari juu ya maisha yako mwenyewe kila siku.
- Wasikilize washauri wema mara kwa mara.
- Shiriki katika sala na maombi.
- Usitengeneze nafasi ya dhambi ya uzinzi hata kidogo. (if you give a devil an inch he’ll take a mile)
- Kuwa mtu wa ratiba
- Epuka kuangalia picha au filamu za ngono.
Jinsi ya kutunza mahusiano.
Kama vile mchi wa mchungwa ili unawili huitaji matunzo, vilevile, mahusiano ili yawebora huitaji matunzo. Kosa ambalo vijana wengi hukosea ni kwamba kuishi mazingira ya ndoa katika kipindi hiki. Mtazamo huu haujawahi kuwa sahihi hata kidogo.
Ili kutunza mahusiano yako usiruhusu kufanya tendo la ndoa, na rafiki yako (girlfriend or boy friend)
Tambua hili;
KWA WASICHANA/WANAWAKE
Wavulana kadhaa wanasema kwamba hawawezi kumwoa mwanamke ambaye wamefanya naye ngono. Kwa nini? Kwasababu wangependa mtu aliye safi. Hivyo baada ya mwanaume kupata alichokuwa anakihitaji, baada ya hilo tendo, upendo wote hufa na kukwona haufai tena.
Acha nikupitishe kwenye kisa kimoja wapo kwenye biblia; 1 Samwel 13:1-17.
Tunaona Amnoni alimpenda umbu lake, Tamari, hadi Kiasi cha kukonda kwa vile alivyo kuwa akimpenda Tamari. Kwanini ee mwana mfalme unakonda hivi siku hizi? hutaki kuniambia? Amnoni akamwambia yonadabu, nampenda Tamari umbu la ndugu yangu Absalobu (1 Sam 13:4). Kwa mtazamo wa haraka haraka jambo hili laweza kudhihirisha kama vile upendo wa dhati mno. Lakini hatima yake ilikuwa ni mbaya mno.
Tatizo huja kwamba vijana wengi huona ya kuwa njia pekee ya kuthibitisha ya kwamba mtu unampenda ni kufanya naye ngono. Hapa tunaona Amnoni anashinikizwa na rafiki yake yonadabu, yakwamba alale na kujifanya yu mgonjwa kisha mfalme ajapo kumwona amwombe amwamuru Tamari aje kumuuguza. Amnoni alifikiri ya kuwa hii ilikuwa ni namna nzuri ya kumpata Tamari asijue ni hasara ya nafsi yake mwenyewe.
Baadaye Tamari anawasili kwa Amnoni. Ili kukamilisha mpango wake, Amnoni alikuwa hana budi kuwaamuru wote watoke nje. Kisha akamshika mkono Tamari na kumsihi kwamba “njoo ulale nami, ndugu yangu” (1 Sam 13:13). Lakini Tamari kwa hekima yake kubwa anaonesha kukataa wito huo kwa mara ya kwanza. Naye akamjibu, la sivyo, ndugu yangu usinitenze nguvu, kwani haifai kutendeka hivi katika israel. Basi, sasa nakusihi, useme na mfalme kwa maana hatakukataza kunioa. Majibu haya yalikuwa ni mazuri mno na yakuigwa sana. Hiki ndicho wanawake hawana budi kuwajibu watu wanaowashinikiza wafanye ngono, ikiwa anadai kukupenda. Kwa sababu ikiwa Amnoni alimpenda Tamari upendo wa kweli na sio wa tamaa, je ni nini kilicho mzuia kumwambia mfalme haja yake ya kumwoa Tamari? (1 Sam 13:12-13)
Vijana wengi leo wamejikita katika kuwadanganya tu mabinti na kuwachafua na sio kuoa. Mtu asiye tayari kuchukua hatua za kuwajuza wazazi wako juu ya haja yake yakuwa na ndoa nawe, huyo hawezi kuwa mme wako bora.
Hatimaye, Amnoni alizidi kumshawishi Tamari kwa maneno ya ushawishi na hata Tamari kukubali. Walakini yeye hakukubali kusikiliza sauti yake, naye akiwa na nguvu kuliko yeye, akamtenza nguvu, akalala naye. (1 Sam 13:14). Kwa nguvu Amnoni akaona alale na Tamari, na Tamari huenda alifikiri ya kuwa huenda mtu huyo alikuwa na upendo kweli. Ni kweli upendo alikuwa nao kwa maana hadi alifikia kukonda, lakini njia aliyoitumia haikuwa sahihi. Kwa maana baada ya kumaliza kufanya naye ngono, alimkataa kwa machukio makuu. Biblia inasema; kisha amnoni akamchukia machukio makuu sana; kwa maana machukio aliyomchukia yakawa makuu kuliko yale mapenzi aliyokuwa amempenda kwanza. Amnoni akamwambia ondoka, nenda zako. Naye akamwambia, sivyo kwa mabaya haya ya kunitoa ni makuu kuliko yale uliyonitendea. Lakini alikataa kumsikiliza. Ndipo akamwita mtumishi wake aliyemtumikia, akasema mtoe mwanamke huyu kwangu ukafunge mlango. (1 Sam 13:15-17)
Hii ndio asili ya wanaume, Amnoni anamfukuza Tamari, upendo ule wa kwanza haupo tena, na hana mpango naye tena, na pia alimfukuza kwa fujo sana kuliko kumkaribisha kwake. Ndugu zangu wanawake, wajueni wanaume vyema sana. Tofauti ya Amnoni na vijana wa sasa ni hii, vijana wa sasa hawana haja ya kukwambia ya kwamba hakupendi, hivyo huendelea kukufariji mdogo mdogo. Hatimaye hatima yake ni kuachika kabisa, na kufukuzwa kwa mafukuzo makuu. Leo kwenye mashule, vyuo, na mitaani jambo hili hutokea kila iitwapo leo, watu hupatwa na majonzi tele kwa sababu hawakujua mambo haya kuhusu mwanaume. Nawaambieni hili wanawake liwe Faraja yenu. Na kama ukibahatika kuanzisha ndoa na huyo mtu, kunahatari ya ndoa kutokudumu.
Je, hilo ni lakushangaza, pengine hata kukuudhi? Basi kumbuka jambo hili: sinema na televisheni hutukuza ngono kati ya vijana na kufanya ionekane kama burudani isiyodhuru au kwamba ndio upendo wa kweli.
Lakini usidanganyike! Wale wanaojaribu kukushawishi ufanye ngono kabla ya ndoa wanatafuta tu faida zao wenyewe;
Ikiwa unashawishiwa kufanya ngono na rafiki yako wa kiume, huku akidai kuwa ni ishara kwamba unampenda ama la, wewe usiogope kwa kuwaza kwamba atakuacha, na kufanya naye ngono. Ikiwa atakuacha kwa sababu ya kukataa kufanya naye ngono, basi huyo hakustahili. (1 kor 13:4,5)
Mwanamme akiisha kulala na mwanamke ni
vigumu kumwoa.
KWA WAVULANA/WANAUME.
Ikiwa unaurafiki wa karibu na msichana, jiulize, je unamjali kweli? Ikiwa jibu lako ni ndio, je unawezaje kuonyesha kuwa unamjali? Kwakua na nguvu kwa kushikamana na sheria za Mungu, hekima ya kuepuka hali zenye kushawishi, na upendo utakaokusaidia kuhangaikia faida zake.
Ikiwa unasifa kama hizo, basi yaelekea mwanamke huyo atahisi kama alivyohisi msichana mshulami mwenye maadili mazuri aliyesema. “mpenzi wangu ni wangu nami ni wake” (wimbo wa Suleimani
2:16)
Mapendekezo kwa wote;
1. Mtu akijaribu kukushurutisha ufanye naye ngono kwa kukwambia “ikiwa unanipenda,
utanikubaria”, mjibu hivi kwa uthabiti: ikiwa kweli unanipenda, huwezi kuniomba nifanye hivyo!
2. Inapohusu mwenendo wako na watu wa jinsi tofauti, sheria nzuri ya kufuata ni hii: ikiwa jambo ambalo hungepennda wazazi wako waone ukifanya, basi hupaswi kulifanya.
Mwanamke na mwanaume kabla ya kuingia kwenye ndoa, Kuna mambo unatakiwa kuyaelewa.
Popote ulipo unatakiwa kutambua kuwa unatakiwa kuwa mkamilifu kwanza na sio Kusubiri ndoa ikukamilishe. Kama umeshindwa kuwa mkamilifu ukiwa peke yako basi huwezi kukamilika ukiingia kwenye ndoa, kiuhalisia hata ndoa yako itakuwa haijakamilika. Kwahiyo jikamilishe madhaifu yako ukiwa peke yako ili ndoa yako iweze kukamilika kwa wakati ujao.
Watu wengi huingia kwenye ndoa kwa sababu mbalimbali, inaweza kuwa kwa sababu ya umri. Wengi wao uhofia kuzeeka hivyo huingia kwenye ndoa ambazo hayakuwa mapenzi ya Mungu. Wengine huingia kwenye ndoa kwa sababu ya msukumo wa wazazi. Lakini ndoa sio jambo la kukurupukia eti kisa kuna jambo limetokea kwenye maisha yako ya duniani Ndoa ni hatua ya juu zaidi ya urafiki hapa duniani, kwahiyo oa au olewa na rafiki yako mtu ambaye unampenda na unamjua vizuri.
SHERIA YA NDOA
Swali msingi sana ambalo mtu hanabudi kujiuliza hapa ni hili; utafunga ndoa na huyu mwanamke au utafunga ndoa na huyu mwanaume? Swali hili huonesha maandalizi msingi ambayo hayanabudi kutiliwa maanani, leo watu wamekuwa wakijiandaa tu katika shughuli mbalimbali zinazowaingiza kipato lakini swala la kuandaa ndoa wamelisahau. Watu wanadhani ya kwamaba watakuwa na ndoa nzuri mara tu baada ya kuoa au kuolewa. Mtazamo huu si sahihi! Ukiangalia vyema utaona tafiti zinaonesha ya kwamba talaka nyingi hutokea miaka ya kwanza ya ndoa. Hii ni kwasababu ya kushindwa kufanya maandalizi mazuri.
Talaka ni matokeo ya kukosa maandalizi ya ndoa na kushindwa kujifunza stadi za kufanya mambo kwa umoja kama marafiki wa ndani sana. Mahusiano ya ndoa ni zaidi ya uhusiano huu wa kawaida, kwa sababau huusisha upendo wa ndani sana (in-love). Kitu ambacho hukatazwa zaidi katika kipindi hiki cha ndoa ni talaka.
Biblia inasema (Mathayo 19:9) Nami nawaambia ninyi, kila mtu atakaye mwacha mkewe, isipokuwa ni kwasabu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini
Hivyo ni mwiko kwa Habari ya talaka kwa wakristo. Kuepuka hili, maandalizi yapaswa yawe sawia. La sivyo, talaka zitazidi idadi ya ndoa zinazofungwa kwa hakika.
Unaweza kupata nakala ambazo zimesomwa na kufanyiwa midahalo kwenye kurasa za mitandao ya kijamii.
YouTube; GLOPEC TV
TikTok; Dominick_mwenda
Instagram; mwl.dominickmwenda
Audiomack; Dominick Mwenda
Email address; dominickmwenda99@gmail.com
WhatsApp number; https://wa.me/255614236148
Imeandaliwa na DOMINICK MWENDA, MWALIMU WA maisha na MWANDISHI wa vitabu vya motisha.

Ni kweli, kabisa....
ReplyDeleteAmina
ReplyDelete