TUKIO LA MAZINDUZI YA KITABU "KABLA HUJASEMA NDIO" KILICHOANDIKWA NA DOMINICK MWENDA
HILI NI TANGAZO RASMI LA MAZINDUZI YA KITABU CHANGU CHA KABLA HUJASEMA NDIO KUHUSU KITABU Kuna maneno ambayo hufungwa kwa pete [ alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitenganishe ] lakini yalianza kwenye macho. Kuna mioyo iliyosema "NDIYO" kwa sauti [Nipo tayari kuwa na wewe] Kabla Haijasema "NAJIELEWA" kwa ukimya. na kunasafari ambazo huanza kwa kushikana mikono lakini huishia kwa kushikana maumivu. kitabu hiki; kinazaliwa kutoka katika maumivu na matumaini. ni sauti ya kweli kwa kila moyo unaotamani uhusiano wa maana, si wa maigizo. KINAGUSA PANDE MBALIMBALI ZA MAHUSIANO KAMA; Wakati sahihi wa kuanzisha mahusiano. Jinsi ya kutibu majeraha ya nafsi yaliyotokana na mahusiano yaliyovunjika. Jinsi ya kukuza upendo kwa mtu unayempenda Jinsi ya kumfanya mtu akupende wewe tu. Jinsi ya kuweka mawasiliano sawa katika ndoa. Lugha za upendo. Jinsi ya kudumisha upendo wa honeymoon siku za maisha yako yote ya ndoa. Kinachofanya watu waingie kwenye mahusiano...