NAMNA YA KUACHA DHAMBI BY DOMINICK
Wote waliochagua kuwa watoto wa MUNGU hawanabudi kuwa najuhudi kuacha dhambi, kwa maana BABA yao ni mtakatifu, nao hawana budi wawe watakatifu! Sasa, twende tuchunguze ni nini tufanye sasa; ikiwa twataka kuacha kutenda dhambi (uovu) lakini hatuwezi!
Soma kitabu cha Warumi 7:14-25. Irudie kuisoma walau mara mbili au mara tatu KWA MSISITIZO WA KIROHO! Umepata kitu hapo? Sasa tuchambue; Paulo anaeleza kwenye aya 14 kwamba; “… kwa kuwa mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi” maneno haya yanaeleza habari ya asili ya dhambi ambayo ni mwili huu.
Mwili ulishakataa kufanya yaliyomema, hivyo wahitaji Roho Mtakatifu ili upate kutenda yafaayo. Hatua ya kumwitaji Roho Mtakatifu ni ya msingi sana kwenye maisha; lakini swali ni kwamba unamwalika Roho kwako; je akaye katika mazingira gani? Wengi wanatamani sana kumpata huyo Roho mtakatifu, ni jambo jema! Lakini, hakikisha kunausafi ndani yako ndipo utakapobakia na ushuhuda wa ROHO! Hangaikia kwanza mazingira ya huyo ROHO kuishi ndani yako! ROHO mtakatifu hupewa kila mtu aliamua kuacha dhambi na kuwa mfuasi wa YESU KRISTO; Soma Warumi 8:14; inasema “kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa MUNGU, hao ndio wana wa MUNGU”!
Soma aya ya 15 na 17; Biblia inasema “maana sijui nilifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda. Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu”. Hapa unapata hili kuwa; ubaya wa mtu, si jinsi alivyo, bali dhambi au uovu ndani yake. Endelea kusoma hadi aya ya 25. Utagundua kuwa; kwako wewe utakaye kutenda mema, kuna sheria ya dhambi, na wala huo uovu si wewe ufanyaye bali ni dhambi ikaayo ndani yako. Kwa ufupi ni kwamba kwako wewe utakaye kutenda lililo jema halikai neno jema, bali lililobaya ndilo likaalo kwako; kwa maana waifurahia sheria ya MUNGU kwa utu wako wa ndani, lakini katika viungo vyako kuna sheria iliyombali na ya MUNGU, inayopiga vita na ile sheria ndani yako na kukufanya mateka wa ile sheria ya dhambi. Umeliona hilo?
Sasa cha msingi ni kujaza mema ndani yako; kwa sababu ikiwa mema yanakaa ndani mwako, dhambi haitapata nafasi na hivyo hakutakuwa na sheria ya mwili ipiganayo na ile ya roho na hata kama ikiwepo, haitakuwa na nguvu! Soma Marko 7: 20-23, inasema; … kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya,.. haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi! Haya yamtokayo mtu ndiyo yaliyojaa ndani yake! Aliyejaa matusi, lazima atatukana! Alijaa upendo, lazima anapenda! Aliyejaa uovu, lazima autende! Aliyejaa wema ni lazima autende! Kwa sababu ya thawabu ndani ya Ibrahimu, kwake kumtoa Isaka sadaka haukuwa mtihani! Je, umegundua kitu hapo? Hapa jiulize maswali wewe binafsi kabla hujaendelea. Unatamani kuacha dhambi? Je, vitu vipi vitajariza wema ndani yako? Vitu vipi vitajaza ubaya ndani yako? Je, ni kitu gani MUNGU anakuhamasisha uelewe katika sehemu hii (ulipoguswa)?
Soma kwanza; 2 mambo ya nyakati 7:14, Isaya 1:18, ufunuo 3:18-22; Bwana asema “nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu ilyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya kupaka machoni pako upaste kuona. Wote niwapendao mimi nawakemea na kuwarudi; basi fanya bidii, ukatubu! Sali nami sala hii, ichukue iwe ya kwako; Ee Yesu wangu nitie nguvu niiache dhambi, nikajalizwe na wema wote ndani yangu, ubaya ukaniondoke. Nipe asubuhi mpya katika matendo yangu; nijalize ROHO wako Mtakatifu ili nisikumbuke tena dhambi, bali wema! Ee Yesu natamani kukujua, ila nimefanywa mateka wa dhambi naomba msaada wako oooh YESU! Nakiri yakwamba nimetenda dhambi, na mbele yako sistahili tena. Ila naomba huruma yako! Nisaidie ee Yesu, wala mwovu asipate nafasi ya kunishtaki kwa dhambi yangu niliyoitenda! Naomba kwa jina lako YESU Kristo! Amina!
MUNGU akusaidie upate kuacha kutenda dhambi!
USIKOSE KUSOMA NAKALA NYINGINE KUTOKA KWENYE PAGE YETU
Imeandaliwa na DOMINICK MWENDA
.png)
Comments
Post a Comment