TUMIA MAOMBI KATIKA KUUJENGA UFALME WA MUNGU DUNIANI. DOMINICK MWENDA


Mungu aliumba ulimwengu kama mwendelezo(extension) na upanuzi(expansion) wa ufalme wa mbinguni, kisha alimwumba mwanadamu autawale ufalme huo katika mfumo wa kimwili(physical realm). Baada ya shetani kumdanganya mwanadamu, aliuchukua kiuhalali ufalme huo. MUNGU MWENYEZI aliona sio vyema ufalme huo kuwa chini ya Ibilisi ilihali alimwumba mwanadamu ili autawale. Hivyo akaona ni vyema ampeleke Adamu wa pili [YESU KRISTO] ili arudishe ufalme huo uliopotea. Tokea wakati huo tulipoupoteza ufalme, ufalme huo hutekwa na watu wenye nguvu katika namna ya kiroho. Maombi ni nguvu kubwa ambayo kila mtu duniani huweza kuwa nayo. Ni yeye tu namna ya kuitumuia kujijenga kiroho ili kuuteka ufalme huo. 

Changamoto ya wakristo wengi wa leo ni kwamba wanaomba kwa kumaanisha sana pale wanapokuwa katika shida na dhiki tu, mara wanapokuwa katika nyakati nzuri hawana habari na maombi. Kitu hiki kimefanya sisi tuingie gharama kubwa. Huenda ungekuwa na tabia ya kuomba hata kwenye nyakati zako za furaha , basi hizo changamoto zisingetokea. 

Soma kitabu cha Esta 3:13. Kosa kubwa ambalo wayahudi walifanya nyakati za Esta ni kutokumwombea mfalme Ahasuero na serikali yake, wakati wanajua wanaishi chini ya himaya yake. Wayahudi hawa ambao walikuwa mateka kutoka Yerusaremu hawakuwa na tabia ya kumwombea mfalme mpaka mfalme akafikia adhimio la kuwaangamiza wayahudi wote kufuatana na mashtaka waliokuwa nayo. Bila shaka tabia yakutokuomba kwa ajili ya mfalme, iliwagharimu Wayahudi hata kama walikuwa waaminifu kwa MUNGU wao. Umeliona hilo? Hivyo pale ambapo hatuombei mambo mbalimbali kwa kina, huweza kupelekea changamoto kubwa zaidi. Wayahudi hao walifanya nini? Waliingia shauri kwamba WAFUNGE na KUOMBA siku tatu kavu bila kunywa maji wala kula chakula. Wasingeingia gharama ya namna hii ikiwa wangekuwa na tabia ya kumwombea mfalme tokea awali. Lakini hata hivyo MUNGU aliwasikia. Jaribu kufikiri ikiwa wayahudi hao wasingeomba mara walipokuwa katika changamoto hiyo, na wangeamua kumlaumu mfalme au kujitetea kwa maneno yao ya kwamba walikuwa hawana kosa. Je wangepona na gadhabu ya mfalme?

Wakristo wengi waleo ni watu walawama kila siku. Tunawalaumu viongozi, tunawasema vibaya; je, umewahi kuwaombea? Dalili ya kwanza ya kanisa lisiloomba ni kulaumu laumu wengine. Watoto wa MUNGU, humsihi MUNGU kuwapigania, na sio kupigana wenyewe maana wanajua udhaifu wao, katika mwili. Kiufupi, palipo na lawama MUNGU huwaacha mwendelee kulaumiana, wala yeye hatawaingilia, mpaka mtakapoamua kumshirikisha yeye kupitia maombi.

Nyakati mbalimbali za kuomba.

Hakuna mipaka ya kuomba; ni muhimu kujua kuwa tunapaswa kuomba kila wakati tunapokuwa na kibali kwa MUNGU wetu. Lakini zipo nyakati kadhaa ambazo usijaribu kumwacha MUNGU, kama ilivyoelezwa hapo chini

#NYAKATI YA KWANZA

Unapokuwa na furaha, amani, utulivu, kipato, neema, nafuu, na faraja.

Usijekuacha kuomba kwa vile upo kwenye hali nzuri ya maisha. Kumbuka kwamba unahitaji kumwomba MUNGU kila siku, kumshukuru kwa kile alichokupa. Changamoto ni hii, watu wengi tuwapokatika hali hii tunaacha kuomba, na hivyo kupoteza nafasi(nguvu) yetu ya kutawala, hivyo mwovu hupata nafasi ya kufurahi nasi na mwisho kutupindua katika nafasi hiyo. Soma kutoka 17:11; Biblia inasema “ikawa Musa alipouinua mkono wake, Israel walishinda, na alipoushusha mkono wake, Amaleki walishinda” kwa tafsiri ya kimaandiko, Musa kuinua mikono ni ishara ya kuomba kwa MUNGU; hivyo twaweza kusema, Musa alipoomba, Israeli walishinda, na alipoacha kuomba Amaleki wakashinda. Unapofurahi leo hakikisha unatengeneza mazingira mazuri juu ya siku ya taabu mbeleni. Au kutengeneza mazingira ya hiyo tabu kutokutokea kwa njia ya maombi.

#NYAKATI YA PILI

Unapokuwa kwenye uchungu, hali ngumu ya maisha, kukataliwa, kuchukiwa, kutothaminiwa, n.k. 

Unapokuwa katika nyakati kama hii ni Dhahiri unahitaji neema ya MUNGU ili ukomboke. Mwombe MUNGU na wala usitegemee kujitetea kwa maarifa yako na nguvu zako za kimwili. Mfano kijibizana na watu, kuchukiana, nk. Kwa namna yoyote utakapotaka kujitetea kimwili wako mwenyewe, MUNGU atakuacha mwenyewe. Katika kisa cha Esta tunaona wayahudi waliona ni vyema kuomba, kuliko kulaumu! Je wewe, kulaumu ni bora kuliko kuomba?

Ndugu yangu;

Omba unapokuwa na nguvu ya kuomba

Omba unapoona unaudhaifu

Omba unapoona kama huelewi uendako

Omba unapolemewa na mizigo mizito

Omba unapohisi kukataliwa

Omba kila wakati, wakati unaacha kuomba, ndio mwovu anapata nafasi ya kukupata.

Omba unapoona mambo yapo sawa, omba unapoona kuna amani.


KUMBUKA.

JAMBO LA KWANZA.

Unaweza ukawa mwaminifu sana mbele ya Mungu lakini kwa sababu ya uvivu wa kuomba, bado mambo mabaya yakakupata na ukashindwa kutoka kwa sababu huna nguvu ya kuyashinda itokanayo na maombi. Soma kisa cha Hana, mke wa Eli [1 Sam 1:1-13]. Hana aliweza kupata kibali kwa MUNGU na kumzaa Samweli kwa sababu aliingia kwenye maombi.

JAMBO LA PILI.

Mungu ametuumba na kutuweka sehemu fulani ili tutawale kimaamuzi, na mambo mengine kwa njia ya maombi. Huenda, Imani za watu wengine zinashuka, amani katika kikundi chenu inapotea, usalama ndani ya taifa unapotea, au kalama za watu fulani hazisongi kwa sababu ya watu fulani kutokusimama katika nafasi zao kama makuhani kuombea mambo hayo. Je watu hao ni wewe?

JAMBO LA TATU

Kulaumu laumu sio njia nzuri ya kujenga ufalme wa MUNGU. Ni heri kuomba msaada wa MUNGU katika kila udhaifu unaojitokeza. Ukiona mtu anamlaumu laumu mtu au uongozi fulani uliokuwa juu yake ujue hauombei.

JAMBO LA NNE.

Mungu wetu ni MUNGU mwenye wivu; ijapokuwa tunamwomba, hatupaswi kujichanganya na miungu mingine, kwa kufanya hivyo tunaonesha kuwa waaminifu kwa Bwana. Tunapopita katika majaribu mazito na kuyashinda kwa njia ya maombi; thawabu yetu huwa ni kubwa mbinguni.

JAMBO LA TANO.

Usikate tamaa kuendelea kuomba kwa kuwa huoni matokeo ya kile unachokiombea. Maana hata maandiko matakatifu husema wazi yakuwa: imewapasa kumwomba MUNGU sikuzote, wala wasikate tamaa [luka 18:1]. Amini tu! Atajibu!

Hasara za kutokuomba.

Unaingia gharama kubwa ambayo haikuwa ya lazima. Soma Esta 4:17 inasema; na Israeli yote ililia sana, maana kufa kulikuwapo mbele ya macho yao. Kwa sababu ya kutokumwombea mfalme huku wakijua mfalme yupo kinyume nao.

Kupoteza nafasi ya kumiliki. Kama nimfuasi mzuri wa maandiko utaona sehemu tofauti tofauti za Biblia zikionesha watu mbalimbali ambao walirudisha/kuupata umiliki wao kwanjia ya maombi. Hana alimpata mtoto Samweli kwa maombi; 1 Samweli 1:1-13, kanisa lilimsaidia petro akiwa gerezani kwa kumwombea kwa MUNGU; Matendo 12:5, Musa aliposhusha mkono(acha kuomba), Amaleki walishinda vita, na Israeli kushindwa.

Unakuwa dhaifu wa Imani, na nirahisi kutekwa na mitego ya shetani. Maombi ni sala yakuongea na MUNGU. Tunapokosa wasaa wakuongea na MUNGU, tunakosa maelekezo na mwongozo kutoka kwake wa nini tukifanye na nini tusikifanye. Soma 2 Fal 1: 1-4; Ahazia aliacha kumwuliza MUNGU na hivyo Kwenda kwa miungu mingine. Elia aliwauuliza wajumbe wa ahazia kuwa “je ni kwasababu Hapana MUNGU katika Israeli, hata mnakwenda kuuliza kwa baal-zebubu?

Changamoto unayoipitia kutokupata uvumbuzi sahihi. Kutoka hapo juu, tunaona kwa sababu ya Ahazia kutokwenda kumwuliza MUNGU wa kweli ilipelekea tatizo lake kuto kupata Suluhu nzuri, mwishowe akafa.

Hivyo ni bora tuelewe kuwa, imetubidi kuomba bila kuchoka wala kukata tamaa. Hatakama unapitia katika dhiki ya namna gani, au mapito gani, usimwache Bwana. Kwa maana tumaini letu halipo kwenye kutokudondoka bali kwenye kuinuka kila tunapodondoka. Tukumbuke safari yetu ni ya kiroho, tunasafiri kwa mwendo wa Imani, njia yetu tuipitiayo inavisiki, mabonde na milima. Tumwombe kila saa Bwana Yesu ili atuvushe na mapito haya.


KUPITIA BLOG YETU HII UNAWEZA KUPATA TENA MASOMO KUHUSU;

VITA KATI YA NURU NA GIZA

MAANA HALISI YA UKRISTO

PRESTIGE OF BEING WITH GOD 

SIRI NYETI KUHUSU MAHUSIANO 

AND OTHER 

Imeandaliwa na DOMINICK MWENDA, MWALIMU WA maisha, na MWANDISHI wa vitabu vya motisha

Comments

Popular posts from this blog

SIRI NYETI KUHUSU MAHUSIANO BY DOMINICK MWENDA

TRUST IN GOD'S TIMING BY ERICA BROWN edited by DOMINICK MWENDA

DOMINICK MWENDA : THE PRESTIGE OF BEING WITH GOD